Feb 16, 2015

DOKII AIBWAGA YANGA SC, ATUA AZAM FC

Msanii nyota Tanzania, Ummy Wenceslaus maarufu kwa jina la Dokii (kushoto) jana alikuwa miongoni mwa Watanzania waliojitokeza Uwanja wa Azam Complex kuishangilia Azam FC ikimenyana na El Merreikh ya Sudan katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Azam ilishinda 2-0.
Lakini katika michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu visiwani Zanzibar, Dokii (katikati ya rafiki zake) alikuwa akiishangilia Yanga  SC japokuwa Azam FC ilikuwepo pia. 
Dokii ni shabiki mzuri wa soka na husafiri hadi nje ya nchi kwenda kuishangilia timu ya taifa inapocheza. Hapa alikuwa Mombasa, Kenya mwaka juzi kwenye Kombe la Challenge akiishangilia timu ya Bara ikimenyana na Uganda katika Robo Fainali ya Kombe la Challenge na kushinda kwa penalti 4-3 baada ya sare ya 2-2.

0 maoni:

Post a Comment