Klabu ya Simba ya Jijini Dar es
salaam leo imefanikiwa kutoa dozi ya msimu kwa maafande wa Tanzania
Prisons, baada ya kuwafunga mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya
Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo mshambuliaji
wa Simba Ibrahim Ajib ndio aliibuka kinara wa kufumania nyavu baada ya
kutupia kambani bao 3 (Hat trick) ambapo katika kipindi cha pili
alipumzishwa baada ya kupewaa kadi njano.
Simba walijipatia ushindi huo
kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 15, dakika 21 na dakika ya 42 kwa
mkwaju wa penati, na kufanya muamuzi wa mchezo huo Odongo ampatie mpira
wake kwa kazi nzuri aliyoifanya.
Baada ya kutengeneza nafasi
nyingi za mabao Okwi naye akaiandikia Simba bao la nne katika dakika ya
74 kabla ya Ramadhan Singano kumaliza kazi kwa kufunga bao la tano
katika dakika ya 82 kufatia kazi nzuri ya Emanuel Okwi.
Kwa ushindi huo Simba inakuwa
imeweka rekodi nzuri ya kufunga mabao mengi katika mchezo huku ikiwa ni
salamu kuelekea mchezo na Yanga wiki kesho Machi 8.
0 maoni:
Post a Comment