Azam FC leo saa mbili usiku itajitupa kwenye uwanja wa AlMerrikh kukwaana na Al Merrikh SC.
Azam FC ambayo ilitua hapa
Khartoum Jumanne 24/2/2015 imekuwa katika hali nzuri tangia kuwasili.
Vijana wa kitanzania wanaosoma hapa Khartoum wamekuwa wenyeji wetu.
Azam FC imekodi Apartment nzima,
tumekuwa tukiishi kama nyumbani, tunapika wenyewe, tuna ulinzi wa
kutosha wa kambi, na walinzi wetu ambao tumesafiri nao toka Dar es
Salaam wakiongozwa na afisa wa usalama wa Taifa wamekuwa wakifanya doria
masaa 24.
Tulipowasili Khartoum, wapinzani
wetu walijaribu kucheza mchezo mchafu wa kutuchanganya kisaikolojia kwa
kuleta mabasi mawili mabovu kutupolea lakini walishangazwa kuona Azam FC
ikiachana na basi lao na kupanda basi lingine zuri lililoandaliwa na
viongozi wa Azam FC waliotangulia siku tatu kabla.
Jana wakati timu inaenda kufanya
mazoezi uwanjani mashabiki wa Merrikh walijipanga barabarani na kurusha
vumbi, makopo, mawe nk lakini polisi waliokuwa kwenye magari maalum
wakisaidiwa na wanajeshi walifanikiwa kuwadhibiti.
Wenyeji wanasema mashabiki wa Merrikh ni wakorofi na wamekuwa na kawaida ya kufanya fujo kwa timu ngeni.
Benchi la ufundi la Azam FC
linaloongozwa na Joseph Omog limesema hawana wasiwasi kabisa kwani
wamewaandaa vijana kwa ajli ya mchezo wa leo.
CHANZO AZAM FC PAGE
0 maoni:
Post a Comment