Mar 9, 2015

10 BORA YA WACHEZAJI WANAOONGOZA KUPIGA CHENGA NA KUTOA PASI BARANI ULAYA RONALDO HAYUPO HATA 20 BORA


messi26032014Naposema “kufanikiwa au kukamilisha chenga” namaanisha kuwa unampiga mtu au watu chenga halafu unafanikiwa kuumiliki mpira bila kupokonywa na kisha kumpasia mwingine au kufunga au kufanya vyovyote vile, Yaani unapiga chenga bila kupokonywa mpira, Sasa hapo nadhani umenipata kwa ufafanuzi huo ili usije kubakia ushangaa hapa. 
Sasa twende kazi…
Najua haujui ila nitakujuza hapa aisee…
Lionel Messi ndie mchezaji aliepiga chenga nyingi kwa mafanikio barani Ulaya kwa zaidi ya misimu miwili iliopita kuliko mchezaji yeyote.
Messi amepiga chenga 258 bila kupokonywa mpira, Kwa hiyo, Messi ndio top dribbler in Europe zaidi ya misimu miwili iliopita.
Eden Hazard wa Chelsea anafuatia kwa ukaribu zaidi akiwa amezidiwa chenga nne tu na Messi.  Hazard ana chenga 254.
Hazard ni mmoja kati ya wachezaji wawili kutoka kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuingia kwenye 10 bora hiyo.Eden Hazard
Mwingine ni Raheem Sterling wa Liverpool mwenye chenga 172 akishika nafasi ya nane.
Lakini katika hali ya kushangaza, mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo hayupo kwenye 10 bora hiyo na wala kwenye 20 bora ya waliopiga chenga na wakakamilisha chenga zao.
Cristiano Ronaldo yeye hajafikisha hata nusu ya chenga za Messi na Hazard kwa hiyo zaidi ya misimu miwili.
Cristiano amepiga chenga 99 kwa kipindi hicho zaidi ya misimu miwili, ambapo imemfanya kuwa nje ya 20 bora kwenye orodha iliotolewa.
Takwimu hizo zinaonyesha jinsi wachezaji wafupi kina Messi, Hazard na Sterling walivyo wachezaji hatari kwenye timu zao kama wachezeshaji wakubwa.
Na hapa ndipo wachezaji kutoka Ligi Kuu ya Ujerumani wanapotamba. Bundesliga imetoa wachezaji sita katika kumi bora ya wapiga vyenga bora barani Ulaya.
Hapa utawakuta kina Arjen Robben (172) na Frank Ribery (175) wote wa Bayern Munich.

Kuna winga Roberto Firmino (244) wa Hoffenheim, Raffael (222) wa Borussia Monchengladbach, Karim Bellarabi (206) wa Bayer Leverkusen, na Eric Choupo-Moting (200) wa Schalke 04.
Lucas Moura wa Paris Saint Germain (PSG) anafunga kumi bora akiwa amepiga chenga 167.
Hakuna mchezaji yeyote kutoka Ligi Kuu ya Italia alieingia kwenye kumi bora ya orodha hiyo.

0 maoni:

Post a Comment