BARCELONA
imepanda kileleni mwa La Liga, baada ya ushindi mnono wa mabao 6-1
dhidi ya Rayo Vallecano jana jioni Uwanja wa Nou Camp.
Barca
sasa inafikisha pointi 62, baada ya mechi 26, ikiishushia nafasi ya
pili, Real Madrid yenye pointi 61, baada ya jana kufungwa 1-0 na
Athletic Bilbao.
Luis Suarez alianza kuifungia Barca dakika ya sita, kabla ya Gerard Pique kufunga la pili dakika ya 49.
Barcelona walipata penalti na Tito akatolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu kwenye boksi.
Lionel
Messi alipiga mara ya kwanza penalti akakosa, lakini refa akamuambia
arudie ndipo akafunga dakika ya 56, kabla ya kufunga tena dakika za 63
na 68 kukamilisha hat-trick yake leo.
Alberto
Bueno aliifungia bao la kufutia machozi Vallevano kwa penalti dakika ya
81 na Dani Alves akatolewa kwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu iliyozaa
penalti hiyo, kabla ya Suarez kuhitimisha ‘pati la mabao’ la Barca kwa
bao la dakika ya 90.
Kikosi
cha Barcelona kilikuwa: Bravo, Pique, Xavi, Pedro, Iniesta/Rafinha dk66,
Suarez, Messi, Mascherano/Rakitic dk66, Alba/Adriano dk76, Alves na
Mathieu.
Rayo Vallecano:
Alvarez, Tito, Amaya, Ba, Insua, Trashorras, Lica/Aquino dk71,
Jozabed/Quini dk66, Bueno, Kakuta, Baptistao/Manucho dk83.
Luis Suarez amefunga mabao mawili katika ushindi wa 6-1 wa Barcelona dhidi ya Rayo Vallecano
0 maoni:
Post a Comment