HIZI ni habari njema ambazo zinaweza kumfariji Angel di Maria.
Mwanasoka
huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa ana msimu mgumu Manchester
United uwanjani, lakini kiwango chake hakijaathiri umaarufu wake nje ya
Uwanja kutokana na jezi kuongoza kwa mauzo katika Ligi Kuu ya England.
Kwa mujibu wa muuzaji wa reja reja wa duka la Sports Direct,
ambaye anauza jezi za timu za Arsenal, Aston Villa, Chelsea, Liverpool,
United, Manchester City, Tottenham na Newcastle, jezi ya Di Maria
inauliziwa na mtu mmoja karibu katika kila wanunua jezi tofauti 10.
Mchezaji ghali wa Manchester United, Angel di Maria anaongoza kwa kuuza jezi katika orodha ya SportsDirect
Di Maria, Sanchez na Costa ndio wamo kwenye tatu bora wote kwa pamoja wakiwa na asilimia 15.66
Jumla
ya asilimia yake ni 9.59 ambayo inamfanya aongoze sokoni, akifuatiwa na
nyota wa Arsenal, Alexis Sanchez, mchezaji huyo wa Chile akiwa nafasi
ya pili kwa asilimia 3.8.
Di Maria amekuwa katika wakati mgumu uwanjani tangu asajiliwe kwa dau la Pauni Milioni 59.7 kutoka Real Madrid.
0 maoni:
Post a Comment