KIUNGO Yaya Toure amesema anafikiria kustaafu soka ya kimataifa baada ya kutimiza malengo yake.
Toure
aliiongoza nchi yake kama Nahodha kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika,
hilo likiwa taji la kwanza kubwa baada ya zaidi ya miongo miwili na sasa
anaweza kufuata nyayo za kaka yake, Kolo kuvua jezi Ivory Coast.
Toure
amesema atachukua siku kadhaa kuamua mustakabali wake, lakini
amependekeza, kizazi kipya sasa lazima kipewe nafasi kikosi cha Tembo.
Toure aliichezea Ivory Coast ikitoa sare na Equatorial Guinea mjini Abidjan Jumapili katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
"Mustakabali wangu?' aliuliza, alipoulizwa na BBC. "Inabidi usubiri. Sasa, malengo yangu yametimia. Tunapaswa kusubiri kwa siku kadhaa na kuona tutafanya nini,".
"Kaka
yangu amestaafu, na Copa (Barry, kipa wa muda mrefu wa Ivory Coast)
naye pia. Muda wa nyota wanaochipukia utafika karibuni. Tunahitaji
kuwaachia wao.
Maneno
haya ya Toure yanaweza kuwa habari njema kwa klabu yake, Manchseter
City, ambayo ilikuwa katika wakati mgumu kwa kumkosa mchezaji huyo
alipokuwa kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika nchini Equatorial Guinea.
0 maoni:
Post a Comment