Mar 21, 2015

MICHAEL CARRICK ASAINI MKATABA MPYA MAN UNITED

KIUNGO Michael Carrick amepata bonge la furaha Manchester United kuelekea mechi na mahasimu wao wakubwa, Liverpool baada ya kusaini Mkataba mpya mwaka mmoja Old Trafford.
Taarifa ya Manchester United iliyotumwa BIN ZUBEIRY imesema kwamba kiungo huyo anabaki kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Louis van Gaal licha ya kukosa miezi miwili na nusu ya kwanza ya msimu kwa sababu ya kuwa maumivu ya kifundo cha mguu, alichoumia katika mazoezi ya kwanza ya Mholanzi huyo Agosti mwaka jana.
Van Gaal amempa Unahodha Msaidizi Carrick, baada ya kiungo huyo kuonyesha mchezo mzuri na kutengeneza bao la kwanza lililofungwa na Marouane Fellaini mwishoni mwa wiki katika ushindi wa 3-0 nyumbani dhidi ya Tottenham kabla ya yeye mwenyewe kufunga.
Carrick has made 17 appearances for Manchester United this seasonĀ 
Michael Carrick ameichezea United mechi 17 msimu huu baada ya kuwa nje mwanzoni mwa msimu kwa sababu ya maumivu ya enka

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 33, aliyejiunga na United kutoka Spurs kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 18.6 mwaka 2006, alitarajiwa kumaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu.

0 maoni:

Post a Comment