TIMU
ya Manchester United imeifunga Sunderland mabao 2-0 katika mchezo wa
Ligi Kuu ya England jioni ya leo Uwanja wa Old Trafford.
Ikiongozwa
na washambuliaji Wayne Rooney na Radamel Falcao, timu hiyo ya Louis van
Gaal ilicheza vizuri na kupata ushindi huo kwa mabao ya kipindi cha
pili..
Refa Roger East
alikuwa kituko pale alipomuonyesha kadi nyekundu Wes Brown badala ya
John O'Shea aliyemuangusha kwenye eneo la hatari Radamel Falcao na
kusababisha penalti.
Nahodha
wa England, Rooney akaenda kuifungia bao la kwanza kwa penalty United
dakika ya 66, kabla ya kufunga la pili kwa kichwa dakika ya 84 na sasa
United inafikisha pointi 50 baada ya kucheza mechi 27.
Kikosi
cha Manchester United kilikuwa: De Gea, Valencia, Smalling, Evans,
Rojo, Blind; Herrera, Young, Di Maria/Januzaj, Rooney/Mata na
Falcao/Fellaini.
Sunderland:
Pantilimon; Reveillere, van Aanholt, Brown, O’Shea, Cattermole,
Larsson, Gomez, Johnson/Fletcher, Wickham/Fletcher na Defoe/Fletcher.
0 maoni:
Post a Comment