TIMU
ya Barcelona imeifunga Granada mabao 3-1 katika La Liga jioni ya leo na
kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara Real Madrid hadi kubaki
moja.
Ivan Rakitic
aliwafungia wageni bao la kuongoza dakika ya 26, kabla ya Luis Suarez
kuongeza la pili dakika ya kwanza kipindi cha pili.
Fran
Rica akaifungia bao la kufutia machozi Granada dakika tano baadaye kwa
penalti baada ya Marc Bartra kumuangusha Lass Bangoura- kabla ya Lionel
Messi kuifungia timu ya Luis Enrique bao la tatu zikiwa zimebaki dakika
20.
Granada: Oier; Nyom,
Babin, Cala, Foulquier; Iturra, Rico, Marquez/Rochina dk67,
Bangoura/Candeias dk79, Ibanez na Cordoba/Isaac 78.
Barcelona:
Bravo; Alves, Bartra, Mathieu/Busquets dk75, Alba, Mascherano,
Xavi/Rafinha dk65, Rakitic, Messi, Neymar na Suarez/Pedro dk79.
Suarez akikimbia kushangilia baada ya kuifungia timu ya Luis Enrique leo
0 maoni:
Post a Comment