Apr 10, 2015

ALVES AFUNGASHA, AWAAGA BARCELONA, ANAKWENDA MAN UNITED AU MAN CITY

BEKI wa pembeni, Dani Alves anatazamiwa kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu baada ya mwakilishi wake kuthibitisha mlinzi huyo wa kulia wa Kibrazil amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
Alves amefurahia mafanikio kwa miaka saba Barcelona, akishinda mataji manne ya Hispania na mawili ya Ligi ya Mabingwa.
Lakini mkonhwe huyo mwenye umri wa miaka 31, hajawa tayari kungeza Mkataba na klabu hiyo ya Nou Camp.
Alves has enjoyed seven successful years at Barcelona, winning four Spanish titles
Beki wa kulia wa Brazil, Dani Alves anajiandaa kuondoka Barcelona msimu huu

Wakala wa mchezaji huyo, Dinorah Santana, ambaye pia ni mke wa zamani wa Alves, amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari jana kwamba mteja wake amekataa ofa ya kuongeza Mkataba.
"Majadiliano yamekwisha," amesema mwanamama huyo.
"Ikiwa wamesema hii ni ofa ya mwisho, kisha (majadiliano yamekwisha).
Habari hizo zinatoa fursa kwa klabu ambazo zimekuwa zikimtaka beki huyo hodari kuanza kumfuatilia kuwania saini yake.
Beki huyo wa zamani wa Sevilla pia ya Hispania, amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Manchester United na Manchester City zote za England, pamoja na Paris Saint-Germain ya Ufaransa.
Brazilian right-back Dani Alves (right) looks set to leave Barcelona this summer
Alves amekuwa na miaka saba ya mafanikio Barcelona, akishinda mataji manne ya Hispania na mawili ya Ulaya

0 maoni:

Post a Comment