KIONGOZI wa Arsenal, Dick Law amesafiri kwenda Argentina kukamilisha usajili wa kinda Maxi Romero.
Mkuu
wa mijadala ya klabu hiyo, amepaa hadi Amerika Kusini kumalizia mpango
wa kumsajili mshambuliaji kinda wa miaka 16, ambaye tayari ameanza
kufananishwa na Lionel Messi.
The Gunners wamepiga hatua katika mazungumzo na Velez Sarsfield juu ya usajili wa Pauni Milioni 4.5 wa kinda huyo.
Arsenal ipo karibu kumsajili kinda wa miaka 16, Maxi Romero kutoka Velez Sarsfield kwa Pauni 4.5
Lakini
dili hilo limekuwa likitiwa ugumu na haki za umilikinwa Romero- hivyo
amelazimika kusafiri hadi Argentina kukamilisha mipango hiyo.
wakala wa Romero na klabu yake, Velez wote wana hisa katika kummiliki mchezaji huyo,ambayo inalketa mkanganyiko kwa Arsenal.
Ligi
Kuu ya England hairuhusu mmiliki wa tatu katika sheria za usajill na
suala hilo lazima limalizwe kama ya mchezaji kwenda kuanza kazi The
Gunners.
Romero
anatarajiwa kubaki na Velez, kwa mkopo, kwa angalau misimu miwili zaidi
kabla ya kwenda England kuanza maisha mapya Arsenal. Nyota huyo kinda hajawahi kuchezea kikosi cha wakubwa cha Velez, bali amekuwa akifanya nacho mazoezi kama mchezaji wa kikosi hicho.
0 maoni:
Post a Comment