Apr 20, 2015

HANS POPPE AWACHOKOZA YANGA, AWAAMBIA; “MTAFUNGWA TUNISIA, NA PIGA, UA MSUVA ATAVAA JEZI NYEKUNDU”.

Na Hemed Kivuyo, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameendeleza wimbi la kuitisha la kuitisha timu ya Yanga baada ya kutamba kwamba winga wa timu hiyo  Simon Msuva ni damu ya Simba ana atatua Msimbazi msimu ujao.
Poppe ameyasema hayo  alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha TAMASHA LA MICHEZO kinachorushwa na kituo cha Luninga cha ITV kila siku ya jumapili saa nane kamili mchana.
Alisema kuwa  kwasasa wataendelea kuitesa timu ya ya Yanga kwakuendeleza wimbi la kuifunga kutokana na wao kuwa na mbinu nyingi za ndani na nje ya uwanja kila wanapokutana  katika michuano yeyote.
Hans Poppe kushoto amesema anaitakia dua mbaya Yanga SC ifungwe na Etoile

Amedai  sababu za kuifunga Yanga mara kwa mara wanazijua na baadhi ya mbinu hizo ni kuwavuruga na maneno kabla ya mchezo na kwamba wapo wachezaji wengi waliyowahi kuitumikia Simba ambao kwasasa wapo Yanga na hivyo kuiona Yanga kama ni Simba B.
``Wale Yanga sisi tunawaona kama ni Simba B kwakuwa wao wanaona kutuchukulia wachezaji wetu ndiyo sifa ya kutufunga jambo ambalo siyo kweli,tutaendelea kupa supu yam awe na kachumbari ya miba mpaka wawache wachezaji wetu``. Alisema Pope.
Alipoulizwa kama wamaechana na harakati za kumuhitaji winga Simon Msuva, Poppe alisema kuwa  bado wanamuhitaji Mchezaji huyo kwakuwa ni `mtoto` wao  na harakati za kumuwinda haziwezi kukoma mpaka hapo atakapovaa jezi Nyekundu za Simba.
``Yule Msuva ni kijana wetu toka siku nyingi tunajua Yule ni Simba damu na na anamapenzi na Simba hivyo lazima tuhakikishe anakuja Nyumbani kucheza Soka`. Alisema Mwenyekiti huyo wa Usajili  asiyeogopa kutoa kauli zenye kuumiza.
Hans Poppe amesema Msuva atavaa jezi nyekundu

Hakuishia hapo aliendelea kuimbea Yanga mabaya ili itupwe nje ya michuano ya Shirikisho na timu ya Etoel du Sahil ya Tunisa katika Mchezo wa marudiano utakaopigwa huko Tunisia wiki mbili zijazo.
``Mimi naomba Mungu Yanga itolewe hata kwakufungwa mabao nane,kwakuwa siipendi hii timu hata kidogo`.Aliongeza.

0 maoni:

Post a Comment