Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm |
YANGAS SC wanarudi kambini leo baada ya mapumziko ya siku moja, kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Stand United kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga SC walilazimishwa sare ya 1-1 na Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika juzi Uwanja wa Taifa.
Na kabla ya kwenda Tunisia katika mchezo wa marudiano, Yanga SC watakuwa na mechi tatu za Ligi Kuu kesho na Mgambo na mwishoni ma wiki dhidi ya Polisi Morogoro na mwanzoni mwa wiki ijayo na Ruvu Shooting.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba timu inaingia kambini leo na habari njema ni kwamba, kiungo aliyekuwa majeruhi, Salum Telela amepona.
“Habari njema ni kwamba kiungo wetu tegemeo, Salum Telela aliyekuwa majeruhi amepona na atakuwepo dhidi ya Stand,”amesema.
Telela alikosekana dhidi ya Etoile Jumamosi kutokana na maumivu ya enka aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City wiki iliyopita.
Kwa ujumla, Ligi Kuu itaendelea mwishoni mwa wiki kwa Mbeya City kuwakaribisha Kagera Sugar, Simba SC na Ndanda FC, Azam FC na Stand United, Polisi Morogoro na Coastal Union Jumamosi, wakati Jumapili Mtibwa Sugar wataikaribisha JKT Ruvu na Prisons watakuwa wenyeji wa Mgambo JKT.
0 maoni:
Post a Comment