May 21, 2015

BONGO MOVIE WAANZISHA TAWI LA YANGA

UWOYA
Hili ni tawi jipya linaloisapoti klabu ya Yanga  mabingwa wapya wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015. Tawi hili kwa sasa ndio limeanzishwa na tayari lina viongozi wa muda ambao wataliongoza  kwa muda pia ili liweze kufikia malengo yake na ya klabu ya Yanga kufika mbali zaidi.
Kundi ili linaongozwa na viongozi wa muda ambao ni
Mwenyekiti wa tawi…..Mike Sangu
Makamu mwenyekiti…….Catty Lupia
Katibu mkuu…………….Jimmy Mafufu
Mtunza fedha…………..Mayasa Mrisho
Kundi hili lina wanachama wengi sana ambao ni wafanyakazi wa kiwanda cha filamu kwa namna moja au nyingine yaani na wadau wa filamu wamo pia. Hadi sasa wanachama ni Vincent kigosi ‘Ray’,  Irene Uwoya,  Mariamu Ismail,  Barafu Suleiman , Saguda George, Haji Mboto, Haji Adam, Chopamchopanga, Jimmy mafufu (katibu mkuu),Lissa Stella , Issa Mussa (Claud), Dullu Mngullu, Idrissa Makupa…Mr. Kupa, Catthy Lupia (makamu mwenyekiti), Mayasa Mrisho (Mtunza fedha),Stanley msungu, Mr Mo, Mike Sangu (mwenyekiti), Stella Nadya , Jini Kabula, Steve Nyerere , Marry Mawigi , Zahoro China  na Badra
Orodha  ni kubwa sana na hata baadhi ya wanamuziki wa dansi wamo pamoja na bongoflevar.Mengi tutawajuza kadili mambo yatakavyokuwa yanakwenda na lini kikao cha pamoja kitakaa.

0 maoni:

Post a Comment