Mandawa (wa pili kushoto) alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu soka Tanzania bara mwezi Novemba mwaka jana
MWADUI
FC imetia chumvi kwenye kidonda cha Kagera Sugar baada ya kuinasa saini
ya mfungaji hatari wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2014/2015,
Rashid Mandawa.
Mandawa
aliyefunga magoli 10 msimu wa ligi kuu uliomalizika mei 9 mwaka huu,
leo amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia matajiri wa madini
mkoani Shinyanga, Mwadui fc.
Wakati
huo huo, kocha mkuu wa klabu hiyo ambaye alikuwa kwa mkopo katika klabu
ya Coastal Union, Jamhuri Kiwhelo ‘Julio’ ameongeza mkataba wa miaka
mitatu (3) kuendelea kuifundisha klabu hiyo.
Julio pia alikuwa anawania na Wagosi wa Kaya baada ya kufaniikiwa kuwanusuru kushuka daraja.
Siku
za karibuni, Mwadui ilimsajili Malegesi Mwanga kutoka Kagera Sugar,
hivyo ni pigo lingine kubwa kwa ‘Wanankurukumbi’ wenye maskani yao
uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.
Kabla ya kujiunga na Mwadui, Mandawa alikuwa anaripotiwa kuwindwa na Simba.
Pia alikuwa na mpango wa kwenda kufanya majaribo katika klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.CLICK HOME KWA HABARI ZAIDI ZA KIMICHEZO
0 maoni:
Post a Comment