May 25, 2015

HUU NDIO UAMUZI WA MAN U KWA FALCAO

 
Frank Lampard, Didier Drogba, Steven Gerrard na Brad Fiedal leo watacheza mechi zao za mwisho katika ligi kuu ya England baada ya miaka zaidi ya 10 kwa kila mmoja wao.
Hata hivyo macho na masikio ya wapenzi wengi wa soka yapo katika kuangalia hatma ya mshambuliaji wa kicolombia Radamek Falcao ndani ya klabu ya Manchester United.

Falcao ambaye alijiunga na United kwa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Monaco, ameambiwa rasmi na United kwamba klabu hiyo haitoweza kumuongezea muda ndani ya klabu hiyo, hii ni kwa mujibu wa mhariri mkuu wa Dailymail – Ian Ladyman.
Falcao ambaye ameshindwa kung’ara na Man United na hivyo kutumia muda mwingi benchi, ameifungia timu hiyo magoli 4 na kutoa pasi za magoli 4.

Kwa mujibu Ladyman, Falcao alikuwa na mazungumzo na kocha Louis Van Gaal kuhusu hatma yake na hata alikubali kupunguza matakwa ya mshahara ili aendelee kubaki Old Trafford lakini haikuwezekana.

Mchezaji huyo anategemewa kucheza mechi yake ya mwisho leo dhidi ya Hull City katika siku ya mwisho ya Barclays Premier League na baada ya hapo atasafiri kwenda kwao kujiunga na Colombia kwa ajili ya michuano ya Copa America.

0 maoni:

Post a Comment