May 25, 2015

KUHUSU CHANONGO KUMALIZANA NA YANGA MENEJA WAKE ANEA

943612_heroa
STORI ya winga Haruna Chanongo kusajiliwa na Yanga imegonga vichwa vya habari nchini, lakini taarifa mpya kutoka kwa Meneja wake, Jamal Kasongo ni kwamba bado nyota huyo hajamwaga wino Jangwani.
Msimu uliopita wa ligi kuu soka Tanzania bara uliomalizika mei 9 mwaka huu, Chonongo alikuwa anaichezea Stand United ya Shinyanga.
“Ni vyombo vya habari, hatujakaa na viongozi wa Yanga zaidi ya kunipigia simu tu!. Amefananua Kasongo na kuongeza: “Tumezungumza na kufika mahala ambapo tumewaacha wajifikirie (Yanga) na sisi tufikirie, lakini bado hajasaini”.
“Sijakaa mezani kuzungumza nao, nilipigiwa simu tu na kiongozi mmoja wa Yanga na muda si mrefu nimewaambia kwamba tunapaswa kukaa mezani”.
Kwanini Kasongo ambaye pia ni wakala wa Mbwana Samatta wa TP Mazembe, anaweka ngumu kumruhusu Chanongo kusaini Yanga?

“Kubwa zaidi kwangu ni mkataba, kuna vipengele ambavyo nataka lazima viwepo, unajua  tunachotazama ni hatima ya mtoto (Chanongo) kwenda mbele zaidi, nadhani kama Chanongo atakaa zaidi ya mwaka mmoja Yanga atakuwa wa hapa hapa, nina ofa nyingi za nje, kwahiyo nataka kujua kama Chanongo atasaini Yanga hatima yake itakuwaje?’ Amesema Kasongo.

0 maoni:

Post a Comment