Siku chache baada ya mshambuliaji wa
kimataifa wa Togo na Tottenham Hotspurs Emanuel Sheyii Adebayor kufichua
siri kadhaa nzito za ugomvi na familia yake, mastaa kadhaa wa Afrika
wamemuunga mkono kwenye hii ishu.
Moja kati ya mapacha wanaoiunda P-Square Peter amemuunga mkono
Adebayor ambapo amemsifu kwa ujasiri wake na jinsi alivyojitokeza kuwa
muwazi na kutoa yanayomsibu maishani mwake.Peter amemuandikia Adebayor kwa kuandika ‘Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayekudai lolote , familia yako inapaswa kuona fahari kuwa na mtoto kama wewe na si kinyume chake ‘.
Nyota wa zamani wa Arsenal Emmanuel
Frimpong kwa upande wake aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter ambapo
amesema kuwa baada ya kusoma kilichomsibu Adebayor anashukuru Mungu
kwani familia yake ni kila kitu kwake .
Nyota wa Chelsea na mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier
Drogba naye alionyesha kumuunga mkono na amemuombea kwa Mungu na anajua
ipo siku familia ya Adebayor itarudi katika msingi wa familia zote ambao
ni Upendo.
Didier Drogba ni mmoja kati ya watu ambao
wamekuwa karibu na Adebayor katika kipindi hiki kigumu na inasemekana
kuwa alizungumza na Adebayor saa chache kabla ya kuandika waraka mrefu
kwenye mtandao wa Facebook .
Adebayor amefichua mgogoro mkubwa ulioko
baina yake na ndugu zake pamoja na mama yake mzazi ambapo amesema kuwa
kilichomfanya afanye hivyo ni kutoa fundisho na picha halisi ya jinsi
ambavyo familia za Afrika zina shinikizo kwa vijana waliofanikiwa.
Dada wa Adebayor anayefahamika aitwae Lucia
amejibu mapigo ya waraka ulioandikwa na Adebayor ambapo amesema kuwa
kila kilichoandikwa na staa huyu wa soka ni uongo na kwa sasa familia
yake haimuhitaji.
0 maoni:
Post a Comment