Klabu
hiyo imethibitisha uhamisho huo leo na Depay atajiunga na United -
iwapo akifaulu vipimo vya afya dirisha la usajili litakapofunguliwa
Juni.
United imesema
kupitia ukurasa wake Twitter: 'Manchester United imefikia makubaliano na
PSV Eindhoven na Memphis Depay kwa uhamisho wa mchezaji huyo, iwapo
akifaulu vipimo vya afya,".
+6
Winga wa PSV Eindhoven, Depay akisherehekea na taji la Ligi Kuu Uholanzi, maarufu kama Eredivisie mwezi uliopita
WASIFU WA MEMPHIS
Kuzaliwa: Februari 13, 1994
Nafasi: Winga
Klabu: PSV Eindhoven 2011-
2014/15 season
Mechi alizocheza: 35
Mabao aliyofunga: 24
"Itategemea na kama atafaulu vipimo vya afya, mpango utakamailishwa mara dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi Juni.'
Kocha wa PSV, Philip Cocu ametangaza hatua ya kikosi chake asubuhi ya Alhamisi.
Mkurugenzi
wa Usajili, Marcel Brands amesemea kupitia tovuti ya PSV; "Tunajivunia
sana juu ya uhamisho huu ujao. Memphis ametokea kwenye mpango wa soka ya
vijana katika akademi ya PSV na ametoa mchango mkubwa kwa timu kutwaa
ubingwa wa Ligi Kuu Uholanzi msimu huu.
+6
+6
Depay akishangilia na taji la Eredivisie na kulia akiichezea Uholanzi katika Kombe la Dunia
0 maoni:
Post a Comment