May 15, 2015

MSHITUKO MAN UNITED, DE GEA AMALIZANA KILA KITU NA REAL MADRID AKARITHI GLAVU ZA CASILLAS

KIPA wa Manchester United, David de Gea yuko mbioni kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu, baada ya kufikia makubaliano ya vipengele binafsi vya Mkataba na Real Madrid, kwa mujibu wa taarifa nchini Hispania. 
Gazeti la Marca limeripoti kwamba kipa huyo mwenye umri wa miaka 24 amefikia makubaliano na vigogo hao wa La Liga katika dili ambalo ameahidiwa mshahara wa Pauni Milioni 4 kwa mwaka, baada ya makato ya kodi, ambalo linaaminika litakuwa la miaka mitano au sita.
Gazeti hilo la Madrid pia limesema kwamba kitu pekee kinachokosekana katika dili hilo ni makubaliano baina ya United na Madrid juu ya ada ya uhamisho ya mchezaji huyo. Inaweza kuwa Pauni Milioni 30.
Manchester United goalkeeper David de Gea looks set for a summer move to Real Madrid
Kipa wa Manchester United, David de Gea anatarajiwa kuhamia Real Madrid msimu ujao

De Gea akiondoka litakuwa pigo kubwa kwa kikosi cha Louis van Gaal, baada ya kuwa na msimu mwingine mzuri Manchester ambao imeshuhidiwa kipa huyo wa Hispania akiteuliwa katika kikosi bora cha mwaka 2014-2015 cha PFA 
Kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid, anatakiwa kwa udi na uvumnba Madrid akazibe pengo la mkongwe Iker Casillas aliyepoteza ubora wake Bernabeu.
Mzuia michomo huyo alionekana Uwanja wa ndege wa Liverpool akisafiri kwenda Madrid Jumatatu kabla ya kurejea mazoezini Jumatano kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya mahasimu, Arsenal.

0 maoni:

Post a Comment