MSHAMBULIAJI Wayne Rooney ataikosa mechi ya timu yake, Manchester United dhidi ya Arsenal Jumapili kutokana na kutopona mguu.
Nahodha
huyo wa United, alilazimika kutoka nje Jumamosi iliyopita timu yake
ikishinda dhidi ya Crystal Palace, na ameshindwa kupata ahueni kuelekea
mechi na Washika Bunduki.
Mchezaji
mwingine aliyetoka nje pia siku hiyo ni Luke Shaw baada ya kuumia
Uwanja wa Selhurst Park na kocha Louis Van Gaal amethibitisha wawili hao
wote wanaweza kukosa mechi zote mbili za kumalizia msimu.
Wayne Rooney ataukosa mchezo wa Manchester United dhidi ya Arsenal Jumapili kutokana na maumivu ya mguu
"Hali si nzuri kwetu, hawawezi kucheza, wote kati yao,"amesema kocha huyo Mholanzi, akizungumza na MUTV. "Ndiyo, ni kitu cha muda mfupi, tutabakiza mechi moja, hivyo nafikiri ni vigumu kwao kucheza tena msimu huu,"
Nafasi
ya Rooney ilichukuliwa na Radamel Falcao baada ya mapumziko wiki
iliyopita, lakini Robin van Persie anaweza kuziba pengo lake dhidi ya
klabu yake ya zamani, Arsenal baada ya kuthibitika yuko fiti.
Mholanzi
huyo ambaye alikosa mechi dhidi ya Palace kutokana na virusi, lakini
ataanza pamoja na Angel di Maria - ambaye pia anarejea baada ya kupona
majeruhi yake.
0 maoni:
Post a Comment