Kikosi cha Simba, rasmi
kimetangaza kumtema kiungo wake Ibrahim Twaha ‘Messi’.
Messi alisajili na Simba
misimu miwili iliyopita, lakini hakupata nafasi ya kutosha kuonyesha cheche
zake.
Ingawa alianza kuonyesha
cheche wakati wa Abdallah Kibadeni, baada ya Zdravko Logarusic kutwaa ‘madaraka,
mambo yalibadilika.
Tokea hapo, Messi huyo
wa Tanga aliendelea kupotea taratibu, hadi Simba ilipomtema.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema, tayari wamempa ruksa.
“Kweli, Twaha tumemuacha
aende. Unajua kama unaona inafikia unalazimika kufanya jambo fulani, basi ni
vizuri kulifanya mapema,” alisema.
Hivi karibuni, Twaha amekuwa akisikika akisema kwambaa ana mpango wa kuachana na Simba, hivyo timu yoyote inaweza kumsajili kulingana na maelewano yao.
0 maoni:
Post a Comment