Rais wa Simba, Evans Aveva amesema suala la kuibinafsisha klabu hiyo linahitaji ungalifu mkubwa katika mambo kadhaa.
Aveva
amesema kuwa Simba inaweza kubinafsishwa lakini lazima uongozi
uhakikishe na kujua thamani ya klabu hiyo ikiwa imeishajiridhisha kama
ubinafsishaji kweli una faida.
“Ni
suala la kitaalamu, lazima kuliangalia na kutathmini. Kama tutapata
uhakika basi ni suala la thamani ya klabu ya Simba. Hapa si kuangalia
majengo, sijui magari na uwanja ambao tunataka tuanze kuujenga.
“Lakini
kuna suala la maana ya thamani ya Simba kama klabu, hili linahitaji
wataalamu waliotulia na kufanya tathmini ya uhakika. Baada ya hapo,
litafuatia suala la wanachama kuelimishwa kuwa nini kinafanyika, zipi
faida zake.
“Wanachama
ndiyo wamiliki wa klabu, lazima waelimishwe na baada ya hapo kuna suala
la katiba ambayo inasema wamiliki wa Simba ni wanachama. Ukiangalia
hapa utaona hili si jambo dogo,” alisema Aveva.
Mfanyabiashara
maarufu nchini, Mohammed Dewji maarufu kama Mo alikuwa ameeleza wazi
nia yake ya kutaka kuinunua Simba kwa asilimia 51 na zilizobaki 49
zitaachwa kwa wanachama wengine wa Simba. Lakini uongozi wa Simba
umekuwa ukisema unalisikia suala hilo kwenye vyombo vya habari tu.
0 maoni:
Post a Comment