Jan 27, 2016

ALICHOSEMA SUAREZ KUHUSU YEYE KUCHEZA TENA ENGLAND

Mshambuliaji hatari wa Barcelona, Luis Suarez amezungumzia uwezekano wa yeye kurudi
nchini England na kuichezea klabu yake ya zamani ya Liverpool, huku akisema kuwa ndio klabu pekee anayoweza kurudi England kwa ajili
yake.

Suarez ambaye aliichezea Liverpool kwa kipindi cha miaka 2 na nusu kabla ya kusajiliwa na
Barcelona ya nchini Hispania ameiambia ESPN kuwa kila mchezaji ambaye alipata kuichezea Liverpool anajua umuhimu wa mashabiki wa
Liverpool Anfield.

Suarez anasema kuwa mashabiki wa Liverpool ni wa pekee zaidi duniani, na kwamba anawakumbuka kila wakati kitu kinachomfanya
awe na ndoto za siku moja kurudi tena Merseyside kufurahia tena maisha na mashabiki hao.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alijiunga Liverpool mwaka 2011 kwa ada ya uamisho wa pauni 22m na katika kipindi cha miaka 2 na nusu
aliifungia Liverpool magoli 94 kabla ya kusajiliwa na Barcelona kwa dau kubwa la pauni 75m.

0 maoni:

Post a Comment