KIUNGO Haruna Hakizimana Fadhil
Niyonzima ameomba msamaha Yanga
SC na kuahidi kutorudia kuikwaza
klabu kwa namna yoyote.
Mwezi uliopita, Yanga SC ilitangaza
kuvunja Mkataba na Nahodha huyo
wa Rwanda kwa tuhuma za kukiuka
vipengele vya Mkataba wake.
Lakini leo katika Mkutano na
Waandishi wa Habari makao makuu
ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam,
Niyonzima ameomba msamaha ili
arejeshwe kundini.
“Ninapenda kuchukua fursa hii
kuomba msamaha kwa uongozi,
benchi la ufundi na wachezaji
wenzangu pamoja na wanachama na
wapenzi. Ninaipenda timu yangu na
ninapenda kuendelea
kuitumikia,
”amesema.
Aidha, Niyonzima amesema kwamba
kulitokea kutoelewana kimawasiliano
na ofisi ya Katibu Mkuu, Dk Jonas
Tiboroha kiasi cha kulifikisha suala
hilo kwenye hatua hiyo.
Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya
Habari na Mawasiliano ya Yanga SC,
Jerry Muro amesema kwamba suala la
Niyonzima limefika katika uongozi
mkuu wa klabu na lipo katika hatua
nzuri.
Ingawa Muro hakuweza wazi, lakini
inavyoonekana muda si mrefu Yanga
itatangaza kuzika tofauti zake na
mchezaji huyo na kumrejesha kundini
rasmi.
0 maoni:
Post a Comment