Apr 5, 2016

MATOLA APONDA MAAMUZI YA TFF

Na Haji balou
Kocha wa timu ya Geita Gold Mine, Seleman Matola, ameponda maamuzi ya Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka Tanzania TFF,
kwa kutoa maamuzi ya kukurupuka ya kuishusha daraja timu hiyo bila kuzingatia haki.

Matola ameiambia Goal, maamuzi hayo yamemsikitisha sana na haamini kama Kamati hiyo ya TFF, imewatendea haki wakazi wa Geita kwani haki hakuna baya lolote walilotenda na walipanda kwa kutumia uwezo wao ndani ya uwanja na siyo hongo.

“Hukumu haiko sahihi, naweza kusema kamati imekurupuka kwa sababu huwezi kuihukumu Geita pasipo kuwa na vithibitisho
vinavyoonekana machoni mwa watu
amesema Matola. Matola amesema anaamini viongozi wake watapambana kwa kukata rufaa ili kutafuta haki yao ambayo inapotea bila ya sababu zozote za msingi na ameiomba TFF kukutana na Kamati yake ili kuweza kulijadili upya
swala hilo kwasababu wametumia garama kubwa ili kuifikisha timu hiyo hapo.

Kamati hiyo ya nidhamu ilizishusha daraja klabu nne za Geita Gold Mine, Polisi Tabora, Geita JKT Kanebwa na JKT Oljoro pia baadhi ya viongozi na wachezaji watimu hizo walikumbana na kurungu la kufungiwa maisha
kujihusisha na mchezo wa soka huku wengine wakisimamishwa kwa miaka 10 na kutozwa faini ya Sh. 10 milioni.

0 maoni:

Post a Comment