May 8, 2016

BODABODA FC YAICHAPA VIJUSO FC BILA HURUMA



Timu ya Bodaboda fc imeibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya Vijuso fc katika mchezo wa mashindano ya ligi ya mbuzi vijana Cup katika mchezo uliopigwa uwanja wa Shule ya Msingi Muungano.

Magoli ya Bodaboda fc yalifungwa na Saidi milasi dakika ya 40, Given ambaye alifunga magoli mawili katika dakika ya 60 na 67 na goli la mwisho lilifungwa na Bakari ng'ang'a huku goli la kufutia machozi kwa upande wa Vijuso lilifungwa na Yuba mocha.

Ligi hiyo itaendelea tena hapo kesho kwa mchezo mmoja kati ya Nangando fc dhidi ya Z fc mchezo utakao pigwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano.

0 maoni:

Post a Comment