Na Haji balou
Ligi ya mbuzi Vijana Cup imeendelea tena hii leo katika mchezo mmoja uliopigwa katika uwanja wa shule ya Msingi muungano kati ya Nangando fc dhidi ya Zfc na umemalizika kwa Zfc kuibuka na ushindi wa goli 3-2.
Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wakusisimua Nangando fc ndio walikuwa wa kwanza kufunga goli kupitia kwa Shadhili lihambamba katika dakika ya 22 goli lililo dumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika, kipindi cha pili kilianza kwa kasi na dakika ya 50 Zfc walifanikiwa kusawazisha kupitia kwa Mustafa Malunda lakini dakika tano baadae Nangando walipata goli la pili kupitia kwa Fadhili Mbwana mnamo dakika ya 70 Zfc walipata goli la kusawazisha kupitia kwa Mussa kisanga lakini Yahaya likule akamalizia msumali wa mwisho baada ya kuifungia Zfc goli la ushindi katika dakika ya 82.
Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Nangando Abduli ngeta alisema wachezaji wake wamejituma lakini mpira ni mchezo wa makosa na bahati haikuwa kwao ndio maana wamepoteza mechi ya leo.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa mchezo kati ya Sido Fc dhidi ya Black stars

0 maoni:
Post a Comment