Na Haji balou
Pamoja na uongozi wa Free State Stars
ya Afrika Kusini kumzuia kiungo wake
mshambuliaji, Mrisho Ngassa kumtoa kwa
mkopo, nyota huyo amewatoa hofu
mashabiki wa Yanga na kuwaambia siku si
nyingi anarejea kwenye klabu hiyo.
Ngassa ameitoa kauli hiyo muda mfupi
baada ya kuwasili nchini kisha kutazama
mechi ya fainali ya Kombe la FA kati ya
Yanga na Azam FC kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar ambapo Yanga ilishinda mabao
3-1.
Ngassa alijiunga na Free State inayoshiriki
Ligi Kuu Afrika Kusini, mwaka jana baada
ya mkataba wake kumalizika Yanga.
Ngassa amesema viongozi wa Yanga ndio waliowafuata Free State kwa ajili ya
kumuomba kwa mkopo ili aiongezee
nguvu timu hiyo katika hatua ya makundi
ya Kombe la Shirikisho Afrika.
0 maoni:
Post a Comment