May 28, 2016

HABARI NJEMA KWA WAKAZI WA TANGA BAADA YA TIMU ZAO TATU KUSHUKA DARAJA

Na Haji balou
KAIMU Katibu Mkuu wa Coastal Union,
Salim Bawazir amesema timu hiyo sasa
itakuwa chini ya usimamizi wa Nassor
Binslum pamoja na uongozi wa Chama
cha Soka Mkoa wa Tanga (TRFA) kwa
ajili ya kuiwezesha kushiriki vyema Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) ili irejee Ligi
Kuu Bara.

Akizungumza na Mwanaspoti Bawazir
alisema: “Tumepata funzo kubwa,
kugawanyika kwetu ndiko
kulikotushusha daraja, sasa hatutakubali
mambo hayo tena, tutahakikisha Coastal
inashiriki kikamilifu Ligi Daraja la
Kwanza na msimu ujao tutarejea Ligi
Kuu Bara.”

Bawaziri alisema BinSlum na TRFA
watashiriki kikamilifu katika suala zima
la usajili wa wachezaji, kocha mwenye
ujuzi na uzoefu na kuilea timu ikiwa
kwenye kanda itakayopangiwa.

“Tunatambua kwamba FDL ni ngumu
kuliko hata ligi kuu ili uweze kufuzu ni
lazima timu iwe na mikakati kabambe
na si ubabaishaji,” alisema Bawazir.

0 maoni:

Post a Comment