May 27, 2016

WACHEZAJI AZAM FC WAPEWA MAPUMZIKO

WACHEZAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika
Mashariki na Kati Azam FC, wamepewa
mapumziko ya wiki tano baada ya
kumaliza mechi ya mwisho ya msimu wa
2015/16 dhidi ya Yanga kwenye mchezo
wa fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam
Sports Federation Cup) juzi jioni.
Azam FC inayodhaminiwa na Benki ya
NMB ambayo ni benki bora kabisa
iliyosambaa kila kona nchini, ilipoteza
mchezo huo wa fainali baada ya
kufungwa mabao 3-1.

Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu
Na mtandao huu mara baada ya
mchezo huo Ofisa Mtendaji Mkuu wa
Azam FC, Saad Kawemba, alisema kuwa
msimu ndio umeisha kwa timu hiyo na
kilichobakia ni kujipanga kwa ajili ya
kupata matokeo mazuri msimu ujao.
“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu
tumecheza mchezo wa fainali, ingawa
matokeo yalikuwa si mazuri haikuwa
malengo yetu, tulipanga kushinda lakini
lazima tukubali ni matokeo ya mpira,”
alisema.

Kawemba alisema wachezaji watamaliza
likizo hiyo Juni 30 mwaka huu na Julai
Mosi wataanza maandalizi ya msimu
mpya.
“Kwa hiyo tutafanya nini kwa msimu ujao,
tutamuongeza nani, tutamtoa nani hayo
tutazungumza baadaye lakini sasa hivi
tunawaomba washabiki wetu wawe
watulivu na tutaendelea kujipanga,”
alisema.

0 maoni:

Post a Comment