May 27, 2016

MUSSA MGOSI ATAJA VITU VIWILI AMBAVYO HAWEZI KUVISAHAU MSIMU HUU

Na Haji balou
Mshambuliaji mkongwe wa Simba Musa Hassan Mgosi kupitia Simba news amesema kuna vitu viwili ambavyo hatavisahau baada ya msimu huu wa VPL kumalizika huku klabu yake ikiangukia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

“Kuna mambo mengi ambayo yametokea kwenye msimu wa 2015-16 lakini kwa upande
wangu, kuna vitu viwili ambavyo siwezi kuvisahau”, amesema Mgosi ambaye hakupata nafasi ya kutosha kucheza msimu huu kwenye kikosi cha Simba.

“Kitu cha kwanza ni mechi kati yetu ya nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Coastal Union. Coastal Union haikuwa timu ya kututoa sisi
lakini kwenye mpira hakuna udogo wa ukubwa wa timu inategemea na maandalizi ya timu, iliniuma sana kutolewa na timu kama Coastal”.

“Kitu kingine kilikuwa ni kufungwa mechi zetu zote mbili na watani wetu wa jadi Yanga, katika uwepo wangu Simba muda wote, hatujawahi
kufungwa na Yanga mara mbili mfululizo kwenye msimu mmoja, niliumia sana”.

0 maoni:

Post a Comment