May 27, 2016

HAYA NDIO MASHINDANO MAPYA YANAYO DHAMINIWA NA AZAM TV

KAMPUNI ya Azam Media Limited leo imeingia Mkataba na Shirikisho la
Mpira wa miguu Tanzania (TFF)
wenye thamani ya Sh.Bilioni 2 kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Ligi Kuu ya Wanawake
Tanzania na Ligi Kuu ya Vijana wa
umri chini ya miaka 20.

Zoezi hilo limefanyika Ofisi za makao
Makuu ya Azam Media Ltd eneo la
TAZARA, Dar es Salaam upande wa
TFF ukiwakilishwa na Rais wake,
Jamal Malinzi na Azam Media
wakiwakilishwa na Mtendaji wake
Mkuu, Muingereza Rhys Torrington.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi,
Torrington amesema Mkataba huo ni
wa miaka mitano na lengo laoe ni
kuendelea kusaidia kuinua michezo
Tanzania.

"Baada ya mafanikio ya awali tukiwa
na Ligi Kuu ya Wanaume na
mashindano mengine, sasa tunapiga
hatua nyingine hatika jitihada zetu
kuchangia maendeleo ya soka nchini
kwa kuingia mikataba ya ligi hizi
mbili,"amesema Torrington.

Kwa upande wake, Malinzi amesema
kwamba Ligi Kuu ya Wanawake
itaanza kwa kushirikisha klabu 10
Agosti mwaka huu na Ligi ya U20
itashirikisha klabu zote za Ligi Kuu ya Wanaume.

"Na Ligi ya U20 itachezwa sambamba na Ligi Kuu ya wanaume, kabla ya mechi za timu za wakubwa,
zitatangulia mechi za vijana. Na kila
timu itasafirisha timu yake ya vijana
kwa mechi za mikoani. Itakuwa ligi
kamili na yenye kanuni
madhubuti,"amesema Malinzi.

0 maoni:

Post a Comment