May 2, 2016

TIMU YA LIKONGOWELE,SIDO FC ZATAMBA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP WILAYANI LIWALE

Mwandae Mchungulike


                                                     SIDO FC Vs BODABODA
                                                         SIDO FC Vs BODABODA
Timu ya SIDO FC Vs BODABODA 
LIWALE,Katika kundi A Jana mei mosi katika ligi ya Mbuzi vijana cup hapa wilayani Liwale ilitimua vumbi katika uwanja wa shule ya msingi Muungano zilikutanishwa timu ya Z.F.C Vs LIKONGOWELE katika kipindi cha kwanza timu ya Likongowele ilikuwa ya kwanza kujipatia goli namo dakika 45 lilofungwa na Twaha Tido na goli lililodumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza mchakamchaka huku kila timu ikisaka goli katika dakika ya 85 timu ya Likongowele iliongeza goli la pili na dakika ya 87 waliongeza goli la tatu lililofungwa na Twaha Tido huku mwamuzi wa mchezo alipopuliza kipenga cha kumaliza mpira dakika 90 matokeo yalikuwa Z.F.C 0-3 LIKONGOWELE.
Kocha wa timu ya Z.F.C alisema wamecheza vizuri japo wamefungwa goli 3 kwake ni jambo la kawaida ni moja ya mcheza na kocha wa Likongowele Juma Mtumbatu alisema kitu kilisaidia kupata ushindi ni mazoezi na wachezaji wake ni watii sana kwa kile anachowafundisha.
Leo mei 2 katika kundi B kulikuwa na mchezo,mchezo uliochezwa katika uwanja wa shule ya msingi Muungano kati ya timu ya SIDO FC Vs BODABODA katika kipindi cha kwanza Sido fc ilioongoza goli 1 lililofungwa katika dakika ya 40 kupitia mchezaji wao Aikosi goli lililodumu mpaka mapumziko.
Dakika ya 49 ya kipindi cha pili timu ya Bodaboda ilisawazisha goli lililofungwa na Faraja na kupelekea mchezo kuwa mkali zaidi huku kila timu ikihitaji kuongeza goli la ushindi katika mchezo huo.
Namo dakika ya 81 timu ya Sido fc kupitia mchezaji wake Mohamedi alipachika goli la pili ambalo Bodaboda walitaka kusawazisha lakini ujanja ulikuwa mdogo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Bodaboda walikubali kichapo cha goli 2 kwa 1.Matokeo yalikuwa SIDO FC 2-1 BODABODA
Kesho mei 3 katika kundi A kutakuwa na mchezo kati ya timu ya MNALANI Vs KOMBAINI mchezo unaotarajia kuwa mkali wa aina yake kwani timu ya Mnalani iliweza kushinda bao 6 huku timu ya Kigamboni iliweza kuicha timu ya Likongowele bao 3 kwa 1.
KUANGALIA MATOKEO YOTE YA LIGI YA MBUZI VIJANA CUP >>BOFYA HAPA

0 maoni:

Post a Comment