Apr 19, 2016

TFF YAMZURUMU MAGOLI KIUNGO WA MBEYA CITY

Na Haji balou
KIUNGO chipukizi wa Mbeya City FC,
Rafael Daudi Alpha  amesema anashangaa hatajwi katikaorodha ya wafunga wa mabao mengi kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara wakati hadi sasa ana mabao sita.
Amesema anashangaa wakati wote
orodha ya wafungaji wa mabao mengi wa
Ligi Kuu inapotolewa jina lake limekuwa haliorodheshwi hata kwenye tovuti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
"Mimi nimefunga mabao sita, lakini
mara zote nimekuwa siwekwi kwenye orodha ya wafungaji wakati wachezaji wengine waliofunga sawa na mimi wanatajwa kila mara," amesema kinda huyo wa miaka 21.
Hata hivyo, nyota huyo aliyecheza
mechi zaidi 23 msimu huu Mbeya
City, amesema hiyo haimkatishi
tamaa kuendelea kufanya kazi yake
kwa nguvu zote kuhakikisha
anaisaidia timu yake ibaki kwenye Ligi Kuu.

0 maoni:

Post a Comment