Apr 18, 2016

HII NDIO REKODI MPYA YA LIONEL MESSI

Na Haji balou
Superstar wa Argentina Lionel Messi usiku wa jana amefikisha magoli 500 katika maisha yake ya soka aliyoifungia klabu yake na timu yake ya taifa baada ya kufunga bao moja wakati Barca ikilala 2-1 nyumbani mbele ya Valencia.
Nyota huyo mwenye miaka 28 alimaliza ukame wa
kucheza dakika 515 bila ya kufunga bao kufuatia kufunga goli hilo akiwa umbali wa mita 10 toka alipo golikipa wa Diego Alves wa Valencia.
Hata hivyo haukuwa usiku wa sherehe kwa Barcelona ambao walijikuta wakidondosha tena
pointi kwenye La Liga na kufanya mbo za ubingwa wa ligi hiyo kuwa wazi kwa timu zote tatu (Barcelona, Atletico Madrid na Real Madrid).
Leo Messi hata hakushangilia bao hilo ambalo limemuweka kwenye vitabu vya rekodi kutokana
na kikosi Luis Enrique kupoteza mchezo huo wakati kilikuwa kikihitaji pointi tatu zilizokuwa muhimu kwao.

0 maoni:

Post a Comment