Jun 22, 2016

YANGA WAMEFIKIA HAPA KUHUSU HASSAN KESSY KUCHEZA MICHUANO YA CAF

Na Haji Balou
YANGA wamewaandikia
barua Simba SC kuwajulisha
kumsajili beki Hassan
Ramadhan Kessy na kuuliza
kama kuna pingamizi lolote
kutoka kwao, na wakati huo
huo nakala zimepelekwa
Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) na Shirikisho la Soka
Afrika (CAF).

Yanga ilishindwa kumtumia
Kessy Jumapili katika
mchezo wake wa kwanza
wa Kundi A Kombe la
Shirikisho Afrika wakifungwa
1-0 na wenyeji MO Bejaia
nchini Algeria, baada ya
CAF kuomba barua ya
kuruhusiwa kwake kuondoka
klabu yake ya zamani,
Simba SC, ambayo
hawakuwa nayo.

Na mara baada ya mchezo
huo, Yanga imewaandika
barua mahasimu wao hao
wa jadi, ikiwa
imeambatanisha Mkataba
wa Kessy na Simba ambao
unaonyesha umemalizika
Juni 15, mwaka huu na
mchezaji huyo alikuwa
sahihi kuingia Mkataba
mpya na klabu nyingine.

Na Yanga imepanga iwapo
hadi kufika Jumatano Simba
haitakuwa na majibu yoyote
ya barua hiyo – wataomba
TFF iwasaidie
kumuidhinisha beki huyo wa
kulia kuanza kazi Jangwani,
maana yake klabu yake ya
zamani haitakuwa na
pingamizi naye.

Na iwapo Simba SC
watamuwekea pingamizi
Kessy, watapaswa kuwa na
hoja za pingamizi ambalo
litasikilizwa na Kamati ya
Sheria na Hadhi za
Wachezaji ya TFF, chini ya
Mwenyekiti wake, Wakili
Richard Sinamtwa.

Na kulingana na uzito wa
suala hilo, inatarajiwa hadi
kufika Ijumaa Kessy
atakuwa amekwishapewa
baraka za kuanza kuitumikia
Yanga.

0 maoni:

Post a Comment