Na Haji balou
Timu ya Real Madrid imethibitisha kuwa nampango wa kumsajili Alvaro Morata kutoka Juventus msimu huu.
Morata alijiunga na Mabingwa wa Italy Juventus mwaka 2014 akitokea Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne (4) uliogharimu Euro million 20 lakini vigogo hao wa Spain wapo tayari kutoa Euro millioni 30 ilikuinasa saini ya staa huyo.
Taarifa za kina zinasema kuwa Real Madrid imewajulisha Juventus maamuzi yao ya kumwitaji mchezaji Alvaro Morata na atajiunga katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo inayonolewa na Zinedine Zidane.
Kwasasa Alvaro Morata yupo kwenye michuaono ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa na amefunga magoli matatu katika mechi tatu nakuisaidia timu yake ya Hispania kuingia katika hatua ya 16 bora.
0 maoni:
Post a Comment