Nov 11, 2014

MAXIMO KUSAJILI VIUNGU KATIKA DIRISHA DOGO.

Baada ya kuona timu yake inasua sua sehemu ya viungo kocha mkuu wa Yanga Marcio Maximo amepanga kusajili viungo mahili katika dirisha dogo ili kuboresha sehemu hiyo.
Yanga tayari imeshapoteza mechi mbili msimu huu, sare moja na kushinda nne ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo yenye timu 14.
Akizungumza baada ya mchezo wao wa juzi walioshinda 2-0 dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Taifa Maximo alisema ana orodha ndefu ya viungo ambao kwa sasa wanahitajika Yanga.
Katika michezo 7 Yanga wameweza kuchapwa mabao 9 na hiyo ni ishara ya wazi kuwa kuna tatizo kubwa katika sehemu ya kiungo.

0 maoni:

Post a Comment