KIPA wa Simba, Ivo Mapunda, juzi Jumapili aliingia uwanjani kucheza dhidi ya Ruvu Shooting huku akiwa amevalia kaushi iliyoandikwa kwa Kiingereza ‘Why us?’ Pia ilikuwa na maandiko ya Biblia ‘Math7:7’ ambayo aliyatolea ufafanuzi.
Ivo ambaye aliibukia kwenye mchezo huo baada ya
kuwa benchi kwa kipindi kirefu akiuguza mkono na nafasi yake ilichezwa
na chipukizi, Peter Manyika.
Aliandika ujumbe huo ili kuonyesha hisia zake
ambapo ule wa ‘Why us?’ ulikuwa na maana ya ‘Kwa nini sisi?’ na ule wa
Math7:7(Mathayo 7 mstari wa 7) ni maneno yaliyopo kwenye Biblia
yanayosema: “Ombeni, nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtapata, bisheni
nanyi mtafunguliwa.”
Alipoulizwa na Mwanaspoti kwa nini aliandika
hivyo, aliyatolea ufafanuzi huku Manyika akimuunga mkono kwa msisitizo
akisema: “Nimeamua kuandika haya namna nilivyoguswa, hivi kwa nini sisi
tu, kwa nini?
“Lakini pia maneno ya Biblia yalikuwa yakinipa
moyo na kuamini ndiyo utakuwa mwisho, kumbe anayeomba na kutafuta hupata
ni hivyo tu.”
Simba iliifunga Ruvu Shooting bao 1-0 ukiwa ni
ushindi wao wa kwanza baada ya kutoa sare sita mfululizo tangu Ligi Kuu
Bara msimu huu ilipoanza.
0 maoni:
Post a Comment