Kocha wa zamani wa timu ya Manchester United David Moyes ametajwa kuwa meneja mpya wa timu ya kutoka Hispania,Real Sociedad.
Kocha huyo mwenye miaka 51, hii ni kazi yake ya kwanza baada ya kutimuliwa kwenye kilabu cha Man U mwezi wa nne mwaka huu, .Moyes anachukua nafasi ya Jagoba Arrasate ambaye pia ametimuliwa na Sociedad baada ya matokeo mabaya na kusababisha timu hiyo kuangukia nafasi ya 15 katika ligi kuu nchini humo, maarufu kama La Liga.
Mkataba wa Moyes na Real Sociedad ni mpaka june mwaka 2016 na kwama mara ya kwanza ataonekana katika mechi ya Deportivo November 22.
0 maoni:
Post a Comment