Mar 19, 2015

BARCA YAISINDIKIZA NA 1-0 MAN CITY EUROPA LEAGUE

BAO pekee la Ivan Rakitic limeipa Barcelona ushindi wa 1-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Rakitic alifunga bao hilo dakika ya 31, akimalizia krosi ya Lionel Messi na sasa Barca inafuzu Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1, baada ya awali kushinda 2-1 England.
Katika mchezo huo, mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero alikosa penalti dakika ya 78 ambayo iliokolewa na kipa Marc-Andre ter Stegen. Penalti hiyo ilitolewa baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Gerard Pique.
Man City imeungana na timu nyingine mbili za England, Chelsea na Arsenal kuaga katika 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa na sasa zote zitahamia kwenye Europa League.
Kikosi cha Barcelona kilikuwa; Ter Stegen, Alves/Adriano dk90, Pique, Mathieu, Alba, Rakitic/Rafinha dk84, Mascherano, Iniesta, Messi, Suarez na Neymar.
Man City: Hart, Sagna, Kompany, Demichelis, Kolarov, Nasri/Navas dk46, Toure/Bony dk72, Fernandinho, Milner/Lampard dk87, Silva na Aguero.
Barcelona completed their two-legged victory over Manchester City to book a place in the quarter-finals of the Champions League
Wachezaji wa Barcelona wakimpongeza Ivan Rakitic baada ya kufunga bao pekee dhidi ya Manchester City usiku huu

0 maoni:

Post a Comment