‘KIBIBI
KIZEE’ cha Turin kimeinuka tena. Habari ndiyo hiyo. Juventus ya Italia
imefuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kufuatia ushindi wa
mabao 3-2 ugenini dhidi ya Borussia Dormund usiku huu Uwanja wa
Westfalenstadion, Dortmund, Ujerumani.
Juve sasa inakwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-1, baada ya awali kupata ushindi mwembamba nyumbani wa 2-1.
Mshambuliaji
wa zamani wa Manchester United, Carlos Tevez aliifungia Juve bao la
kwanza dakika ya tatu, kabla ya Alvaro Morata kufunga la pili dakika ya
70 kwa pasi ya Muargentina huyo.
Tevez
aliyewahi pia kuchezea Manchester City, aliifungia Juve bao la tatu
zikiwa zimesalia dakika 10 na hicho kinakuwa kipigo cha nne kwa
Dortmund katika mechi nne walizokutana na Juventus kwenye michuano ya Ulaya.
Timu
nyingine zilizotinga Robo Fainali ni PSG, Monaco zote za Ufaransa,
Atletico Madrid, Real Madrid, Barcelona, FC Porto na Bayern Munich.
Droo ya Robo Fainali itapangwa Ijumaa Saa 7:00 mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Carlos Tevez akipongezwa na wenzake baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Borussia Dortmund usiku huu
0 maoni:
Post a Comment