Mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester City
watamuuza Yaya Toure msimu huu katika
mpango unaolenga kuwauza wachezaji wengine
wa kilabu hiyo kwa lengo la kununua wachezaji
chipukizi watakaoongozwa na mchezaji Kevin De
Bruyn wa Wolfsburg.
Kushindwa kwa kilabu hiyo na Barcelona katika
mechi ya kufuzu kwa robo fainali ya kombe la
vilabu bingwa Ulaya kumethibitisha kwamba
mabadiliko makubwa yanahitajika katika kilabu
hiyo.
Katika wachezaji kumi na moja walioanzishwa
katika mechi dhidi ya Barcelona ni Sergio
Aguerro mwenye umri wa maka 26 aliye chini ya
umri wa miaka 27.
Huku Aguerro,Joe Hart,Vincet
Kompany,Fernandinho na David Silva wakiwa na
maisha marefu katika kilabu hiyo ,waliosalia
huenda wakauzwa.
Hii inamaanisha kwamba Yaya Toure,Bacary
Sagna,Martin Demichelis,Alkesandar Kolarov
,Samir Nasri na James Milner ambaye kandarasi
yake inaisha hatma yao haijulikani.
Kati ya wachezaji ambao hawakuanzishwa katika
uwanja wa Nou Camp siku ya jumatano
usiku,Gale Clichy,Pablo Zabaleta,Jesus
Navas,Fernandinho,Steven Jovetic na Edin Dzeko
huenda pia wakauzwa.
Frank lampard amesema kuwa anaondoka ili
kujiunga na kilabu ya New York City nchini
Marekani.
0 maoni:
Post a Comment