Unakumbuka ile skendo iliyompata bondia wa ngumi nchini Francis Cheka baada ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?
Taarifa iliyotolewa na kocha wake Abdalah Komando
na kuthibitishwa na wanafamilia yake inasema Bondia huyo nyota zaidi
nchini sasa ameachiwa huru na atakuwa akitumikia kifungo cha nje.
Alisema Cheka ameachiwa huru baada ya
kushinda rufaa yake aliyokata kupinga kifungo cha miaka mitatu gerezani
na sasa anatumikia kifungo cha nje.
Tayari Cheka alianza kutumikia kifungo
hicho mjini Morogoro lakini taarifa za uhakika zinasema ameachiwa leo
baada ya kushinda rufaa hiyo.
“Tayari ameachiwa, Ila tayari yuko nje,
tunashukuru kwa hatua hii lakini bado kesi yake inaendelea kwa kipindi
chote cha miaka mitatu” alisema kocha wake Abdalah Komando
Cheka alihukumiwa kwenda jela baada ya
kumuumiza meneja wa baa yake mjini Morogoro akimtuhumu kumsababishia
hasara katika baa yake.
0 maoni:
Post a Comment