Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema
pamoja na ushindi wa mabao 5-1, kamwe hawatatanguliza dharau watakapokuwa
ugenini dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.
Pluijm raia wa Uholanzi amesema timu nyingi
dunia zimewahi kuanguka licha ya kuwa zilitangulia kupata ushindi mnono kwa
sababu ya dharau.
“Unaweza kusema sisi ndiyo tunaopaswa kuwa
makini zaidi hata kuliko wao. Kweli tumeshinda tano nyumbani, lakini tuna
uhakika gani wao hawawezi kushinda.
“Lazima tuamini kupita kwetu kutahakikishwa na
mechi ya pili. Dakika 90 bado hatuazimaliza.
“Nimezungumza na wachezaji lakini hili
nitaendelea kulikumbusha tena na tena,” alisema Pluijm.
Yanga ilionyesha kiwango cha juu katika mechi hiyo Jumapili na kufanikiwa kuwaangusha Wazimabwe hao kwa kipigo cha hatari.
0 maoni:
Post a Comment