Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
YANGA SC inashuka dimbani leo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar kujaribu kurudi kileleni mwa LIgi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini itawakosa wachezaji wake sita tegemeo.
Hao ni beki Kevin Yondan, kiungo Said Juma ‘Kizota’na mshambuliaji Danny Mrwanda, ambao kila mmoja ana kadi tatu za njano na klabu haijawaombea kucheza mechi hiyo.
Kanuni mpya ya Ligi Kuu inaruhusu klabu kumuombea mchezaji mwenye adhabu acheze mechi inayofuata ili aje kukosa mechi za baadaye, lakini Yanga haijajisumbua kufanya hivyo.
Aidha, kiungo mwingine Haruna Niyonzima atakosekana leo kwa sababu anatumikia adhabu ya kadi nyekundu, wakati beki na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na kiungo Andrey Coutinho wao bado hawajapona sawasawa maumivu yao.
Yanga SC yenye pointi 31, inahitaji ushindi katika mechi ya leo, ili kurejea kileleni, kufuatia juzi mabingwa watetezi, Azam FC kuifunga Ndanda FC 1-0 na kufikisha pointi 33.
Baada ya mchezo wa leo, Yanga SC itaondoka kesho Dar es Salaam kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji, Mgambo Shooting.
Mara tu baada ya mechi na Mgambo, Yanga SC watageuza Jumapili kurejea Dar es Salaam na Jumatano ijayo watacheza mechi nyingine ya Ligi Kuu ya dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa.
Machi 29, kikosi cha Yanga SC kitakwea ‘pipa’ kuelekea Bulawayo, Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Kwanza, Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya wenyeji, Platinum FC utakaopigwa kati ya Aprili 3 na 5.
Yanga SC itakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na mtaji mzuri wa ushindi wa mabao 5-1 katika mchezo wa kwanza Jumapili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ya marudiano, itachezeshwa na marefa Helder Martins de Carvalho, Jerson Emiliano dos Santos, Wilson Valdmiro Ntyamba na Joao Amado Goma wote wa Angola, wakati Kamisaa atakuwa William Makinati Shongwe kutoka Swaziland.

Beki tegemeo wa Yanga SC, Kevin Yondan atakosekana katika mchezo wa leo kwa sababu ana kadi tatu za njano |

0 maoni:
Post a Comment