DILI
la Manchester United kumnasa Edinson Cavani kama linaelekea kubuma,
baada ya leo asubuhi klabu yake, Paris Saint-Germain kukanusha kwamba
wana mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo.
United
imekuwa ikimfukuzia nyota huyo wa Uruguay katika jitihada za kuiongezea
makali ya safu yake ya ushambuliaji, huku ikitaka kumrejesha Radamel
Falcao klabu yake Monaco ilipomchukua kwa mkopo, na kumtema mkongwe
Robin van Persiealiyeoteza makali.
Lakini
mmiliki wa PSG, Nasser Al-Khelaifi amesema mabingwa hao wa Ufaransa
wana dhamira ya kumbakiza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 na
hawafikirii kumuuza.
PSG imesema haina mpango wa kumuuza Edinson Cavani, maana yake Manchester United hawawezi kumpata mshambuliajin hyo tena
"Edinson
Cavani ni mchezaji ninayempenda haswa,"amesema tajiri huyo. "Naweza
kukuambia kwamba yuko sana nasi, na swali la kuondoka kwake halijatokea.
Paris inampenda, naye anaipenda Paris,".
PSG
ina shaka na mshambuliaji mwingine nyota, Zlatan Ibrahimovic anaweza
kuondoka, ndiyo maana haifikirii kumuuza Cavani iliyemsajii kwa Pauni
Milioni 50 kutoka Napoli mwaka 2013.
0 maoni:
Post a Comment