Apr 13, 2015

YANGA YACHEMSHA KUIPIKU AZAM

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
“Azam ilitwaa ubingwa wa Bara msimu uliopita ikikusanya pointi 62 huku ikimaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja.’
WAMECHEMSHA! Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na ukweli kwamba Yanga SC licha ya kuwa na moto mkali msimu huu, haitaweza kuzifikia pointi ambazo Azam FC walizipata msimu huu hata kama ikitwaa ubingwa msimu huu na kushinda mechi zote tano zilizobaki.
jam
Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, kwa sasa wanaoongoza msimamo wa Ligi Kuu ya Bara wakiwa na pointi 46 baada ya mechi 21, zikiwa zimebaki mechi tano kabla ya msimu huu kufikia tamati Mei 9, mwaka huu.
Azam FC walitwaa taji la kwanza kwao la ligi hiyo msimu ulioipita wakiifikia rekodi ya Simba SC ya kumaliza msimu bila kupoteza mechi hata moja, kikubwa wakikusanya pointi 62 baada ya mechi zote 26.
Kwa mantiki hiyo, Yanga SC yenye pointi 46 kwa sasa ikishinda mechi zote tano zilizobaki itatwaa ubingwa ikiwa na pointi 61, moja pungufu ya pointi za Azam FC za msimu uliopita.
Wakiwa na Mcameroon Joseph Omog, aliyerithi mikoba ya Muingereza Stewart Hall katikati ya msimu, walishinda mechi 18, sare nane. Wakafunga mabao 51 na kuruhusu nyavu zao kutikiswa mara 15.

0 maoni:

Post a Comment